Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, alisema jana Jumatano kuwa ndani ya siku chache, maelfu ya watu wa Gaza wameuawa na kuongeza kuwa: Mafuta bado hayaruhusiwi kuingia Gaza na maji "ni machache sana" na kwamba kuna uhaba wa dawa na vifaatiba mahospitalini.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameyataja mashambulizi ya utawala ghasibu wa Israel huko Gaza kuwa ni makosa ya waziwazi na akaongeza: Ninaitaka Israel iheshimu sheria za vita.
342/